Na CCM Blog, Dar es Salaam
Serikali imeagiza kukamatwa mmiliki wa jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo na kusababisha maafa makubwa ikiwemo kusababisha vifo vya watu 16 hadi sasa huku jumla ya watu 86 wakiokolewa kati yao watano wakiendelea na matibabu, ili asaidie kujulikana chanzo cha kuporomoka jengo hilo.
Pia imeagiza binti mmoja aliyetajwa kwa jina ma Jenifer Jovin maarufu kwa ajina la Niffer, naye akamatw ili aeleeze nani alimpa kibali cha kuchangisha umma, amekusanya fedha kiasi, fedha hizo amezipeleka wapi na kwa nini amefanya hivyo, huku ikitoa mwito kwa Watanzania kuacha kuchangisha fedha wananchi kwa kuwa upo utaratibu rasmi wa utoaji wa misaada kupitia Kamati ya Maafa iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na akaunti hiyo iko Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Maagizo hayo yametolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana Novemba 18, 2024 alipokagua mwendelezo wa kazi ya uokoaji katika jengo hilo lililoporomoka Novemba 16 Kariakoo Jijini Dar es salaam., huku akisisitiza kuwa kazi hiyo ya uokoaji ni endelevu hadi atakapookolewa mtu wa mwisho.
Waziri Mkuu amesema wakati uokoaji ukiendelea tayari Serikali imeunda timu ya watu 19 ya uchunguzi ikiwa ni utekezaji wa agizo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, la kufanya ukaguzi wa chanzo cha kuporomokaa kwa jengo hilo, timu amabayo pia itakagua uimara wa majengo yote yaliyojengwa na yanayoendelea kujengwa katika eneo lote la Kariakoo.
Your Ad Spot
Nov 19, 2024
Home
featured
Kitaifa
SERIKALI YAAGIZA KUKAMATWA MMILIKI GHOROFA LILILOPOROMOKA KARIAKOO, BINTI ALIYECHANGISHA FEDHA MATATANI
SERIKALI YAAGIZA KUKAMATWA MMILIKI GHOROFA LILILOPOROMOKA KARIAKOO, BINTI ALIYECHANGISHA FEDHA MATATANI
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇