LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 3, 2024

RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA GHARAMA ZA MATIBABU KWA WATOTO KUTOKA FAMILIA ZISIZO NA UWEZO WENYE UGONJWA WA MOYO

 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo  akitoa cheti cha shukurani kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB kwa mchango wao wa shilingi bilioni moja katika harambee ya kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku  jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zungu wakiingia ukumbini  katika harambee hiyo. 
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na sehemu ya timu ya wataalamu iliyoongozwa na  Prof. David Mwakyusa (wa tatu toka kushoto nyuma), ambaye akiwa Waziri wa Afya, yeye Profesa Mohamed Janabi (hayupo pichani) na timu hiyo walitoa mchango mkubwa katika kuanzishwa kwa Taasisi ya JKCI mwaka 2015. 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo  akitoa cheti cha shukurani kwa mwakilishi wa taasisi ya kimataifa ya BAPS Charities tawi la Tanzania kwa mchango wake wa dola za Kimarekani laki nne (takriban shilingi 1,078,674,800) katika harambee hiyo.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo  akipokea kuto9ka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila zawadi ya picha ya kuchora ikimuonesha akimpa pole mtoto wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati huo huduma zikipatikana MOI. 

 Sehemu ya wadau waliohudhuria katika harambee aliyoongoza Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku  jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages