Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amepongeza Mpango wa Maendeleo 2025/2026 namna ambavyo serikali imeutekeleza.
Akizungumza jijini Dodoma leo Novemba 5,2024 Mtaturu amesema kuwa mwaka huu wa mwisho wa mpango wenyewe ni kujipima namna ambavyo umefanyika.
Mtaturu amesema kuwa pato la taifa limeongezeka kila mwaka hali inayoonyesha mwenendo mzuri wa mpango wa maendeleo unaotekelezwa .
Ameongeza kuwa SGR imeanza kuonyesha matokeo chanya hivyo ni vizuri ikamaliziwa vipande vilivyobaki kwani itaongeza shughuli za uchumi kwa kusaidia watu kutumia gharama ndogo kufika mbali na muda kidogo.
Aidha amesema kuwa kilimo kinagusa watu wengi na kipaumbele kimojawapo cha mpango huu ni kuhakikisha kunakuwa na uchumi shindani ambao ni shilikishi kwa wananchi hivyo mbolea, pembejeo nyingine kama mbegu na utafiti wa wapi panafaa kwa kilimo kipi na kushauri mpango uje na jibu wa kilimo cha tija ambacho ni cha umwagiliaji si kutegemea mvua.
Sambamba na hilo amegusia suala la DP World ambapo amekiri kuwa matokeo yake chanya yameonekana kwa muda mfupi kwa kupunguza meli kusubiri muda mrefu na mapato yameogezeka ambayo kwa Tanzania ni mafanikio makubwa.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇