Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Serikali bungeni, William Lukuvi (kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo baada ya bunge kujadili na kushauri na hatimaye kupitisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleowa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 pamoja na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwaMwaka wa Fedha 2025/2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Serikali bungeni, William Lukuvi (kulia) akijadiliana jambo na Mbunge wa Makambako, Deo Sanga bungeni Dodoma.
Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Isimani, Iringa akijadiliana jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari.
Lukuvi akizungumza jambo na Waziri wa Maji, Jumaa Awesso.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇