LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 7, 2024

MAKALLA: CCM TUTATUMIA 4R ZA RAIS DK. SAMIA KAMPENI ZA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, AWATAKA WAPINZANI NAO KUZITUMIA

Tabata, Dar es Salaam

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi CPA Amos Makalla, amesema CCM kampeni zake za Uchaguzi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji kwa kutatumia 4R za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Amesema kwa kutumia 4R hizo za Rais Dk. Samia, CCM itafanya kampeni hizo kistaarabu na kuheshimiana kwa lengo la kuimarisha utulivu, amani na mshikamano nchini.


Amesisitiza kuwa viongozi na wanachama wa CCM watakaopata fursa ya kuzungumza katika majukwaa ya kampeni za uchaguzi huo, watajikita kueleza maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia katika vijiji, vitongoji na mitaa.


CPA Makalla ameyasema hayo wakati akizungumza na maelfu ya viongozi na wanachama wa CCM, katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Mwigo Tabata, Ilala jijini Dar es Salaam, jana.


Alisema huo ndiyo msimamo wa CCM kuelekea Uchaguzi huo wa Seikali za mitaa, vitongoji na vijiji, unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

   

"Uchaguzi huu utaongozwa na 4R za Mheshimiwa Rais ambazo ni Maridhiano (Reconciliation), Ustahamilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms), na Kujenga upya Taifa (Rebuilding). CCM inaahidi kufanya kampeni za kistaarabu, hivyo tunaviomba vyama vingine kampeni zitakapoanza, twendeni na hizi 4R.


Tujenge hoja na tutofautiane kwa itikadi kwani tuna Tanzania moja, Uchaguzi uiache Tanzania ikiwa moja yenye amani na utulivu. CCM tunavyosema ndiyo tunamaanisha", alisema CPA Makalla na kuongeza;


"Kwa mambo yaliyofanywa na Serikali ya Rais Dk. Samia, kila mwana CCM akipewa nafasi ya kuongea jukwaani ataongea mambo mengi yaliyofanywa. Kwa hiyo kwetu sisi matusi, kejeli haitokuwa sehemu yetu."

CPA Makalla akizungumza na maelfu ya viongozi na wanachama wa CCM, katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Mwigo Tabata, Ilala jijini Dar es Salaam, jana.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages