Na Lydia Lugakila, Bukoba
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ally Hapi amewataka wanachama wa CCM Mkoani Kagera kutofanya mzaha katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwani viongozi wa mitaa ndio msingi maendeleo ya Watanzania.
Hapi alisema hayo Novemba 20,2024 wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho za kuwatambulisha wagombea wa vijijini 662,mitaa 66 na vitongoji 3664 wa mkoa wa Kagera wanaotarajiwa kushiriki kinyanganyilo cha uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu.
"Hawa ndio watu wa mwanzo kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yetu ya mitaa na vitongoji,hawa ndio wa kwanza kuwapelekea shida zetu,ndio viongozi wakusimamia maendeleo yetu mita hivyo tusifanye mzaha wala ushabiki katika uchaguzi huu tuchague viongozi wenye uwezo wa kuongoza ambao wanatokana CCM"alisema Hapi
Uchaguzi huu ni muhimi sana ata jikoni hauwezi kupika na figa moja hivyo kuanzia ngazi za tawi mpaka Taifa viongozi wanaotokana na Rais makini anayesikiliza watu
Alisema viongozi wa CCM wamechuchujwa kitaalam hao ndio askari wa Dk. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwenyekiti wa cha hicho Taifa hivyo tuchague ccm yenye sera ya kuwaunganisha watu,pasipo ubaguzi,chenye historia na akina ubaguzi wa kikanda wala ukabira,kinachojua uongozi,katika uchaguzi huu ata ule wa mwaka kesho tuchague CCM.
Alisema maendeleo ni kama mpira hivyo tusichanganye wachezaji kutoka vyama vingine ambavyo havijui maendeleo yamefikia wapi hkwahiyo tuchague viongozi wanaosomana,kuelewana na kusikilizana ambao wanatokana na CCM.
Alisema CCM imetekeleza Ilani yake ambapo imetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo vituo vya Afya 485 vyenye uwezo wa kufanya upasuaji nchi nzima na ametengqp shilingi Trilioni 23 kwa ajili ya kufikisha treni ya umeme nchi DRC Kongo hivyo msifanye majaribio chague ni viongozi wanaotokana na CCM ili tuendelee kupata maendeleo maana hao ndio wenye uwezo wa kumfikia Rais Dk.Samia.
Kwa upande wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Nazir Karamagi aliwashauri wananchi kutofanya mzaha katika kuchagua kwasababu viongozi aa Serikali za mitaa ndio msingi wa uundaji wa Serikali kuu hivyo wakifanya makosa wanapotea na kujinyima maendeleo.
Kwa upande wa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Stephen Byabato alisema sababu ya viongozi wa CCM kuchaguliwa inaonekana kwani Rais Samia ameleta maendeleo kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 60 katika Manispaa ya Bukoba kwa ajili ya maendeleo hivyo ni haki kuchagua CCM.
Your Ad Spot
Nov 23, 2024
HAPI: KAGERA MSIFANYE MZAHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇