LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 23, 2024

DEREVA WA BAJAJI NA ABIRIA WAKE WANNE WAFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI KUGONGANA NA LORI

Polisi, Songwe
Dereva wa bajaji yenye namba za usajili MC. 783 DUF aina ya TVS na abiria wake wanne wamefariki dunia baada ya bajaji hiyo kugongana na lori  yenye namba za usajili  T. 958 BCS aina ya Scania mkoani Songwe.  

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Augustino Senga amesema, ajali hiyo imetokea jana, Novemba 22, 2024 saa 3:15 usiku wakati bajaji hiyo lilikuwa likitokea barabara ya Mji mdogo wa Mpemba kuelekea Mji wa Tunduma na kujaribu kuyapita magari mengine yaliyokuwa mbele yake kisha kugongana na lori hilo.

Bajaji hiyo ilikuwa ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Hakimu Kalinga Mkazi wa Muungano Mjini Tunduma na kusababisha vifo hivyo, waliofariki pamoja na dereva huyo wa bajaji ni Rehema Christopher  Sikamnga, (25) Mkristo Biashara, Mfipa  Mkazi wa Msongwa, Festo Aron Mambwe (57) Mkristo Msafwa Mkulima Mkazi wa Mbeya, Rosemary Njema (44) Mkristo Mmalila Mkulima Mkazi wa Ipito Tunduma Na Milembe Siyantemi (36) Mkristo Msukuma Mkulima Mkazi wa Kapele.

Marehemu hao wamehifadhiwa katika Kituo cha Afya Tunduma kilichopo Wilaya ya Momba na chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na Dereva wa Scania anatafutwa. Jeshi la Polisi Mkoa Songwe linatoa wito kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kukagua vyombo vyao kabla ya kuanza safari na kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wote.


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages