LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 5, 2024

2025, CCM TUNAMGOMBEA MMOJA TU KWENYE URAIS NAE NI DKT SAMIA SULIHU HASSAN



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla akizungumza na Wanachama pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo katika Ukumbi wa Ubungo Plaza  , leo NOV 05, 2024, amesema Mwaka huu tuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na tayari Kura za maoni zimepigwa sasa Viongozi wa ngazi ya Mtaa, Vijiji na Vitongoji wanatarajiwa kuchaguliwa Ili kuungana na viongozi waliopo ili kuendelea kuleta maendeleo kwa Wananchi.

CPA Makalla amesisitiza Uchaguzi huu ukiisha Viongozi wataungana na Madiwani na Wabunge pamoja na Rais katika kuleta maendeleo kwani Uchaguzi wa Madiwani na Wabunge bado mpaka mwakani muda utakapofika utatangazwa lakini kwenye Urais CCM inamgombea mmoja tu nae ni Dkt Samia Suluhu Hassan.


"Mtakaposhinda Uchaguzi nyinyi Mhe Rais, Wabunge na Madiwani wanawasubiri maanake nyie ndio mnashirikiana katika kuwaletea Wananchi maendeleo, Madiwani tunao mpaka Mwakani muda utakapofika nafasi zitatangazwa na Wabunge hivyohivyo

 "Ila kwa Urais haihitaji digrii kuelewa kwani Mgombea wetu wa Urais mwakani ni Dkt Samia Suluhu Hassan ambae atashirikiana na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji,Madiwani na Wabunge katika kuleta maendeleo na anawasubiri pindi mkataposhinda na ushindi huu utakuwa ni wa heshima kwake Dkt Samia kwa kazi nzuri alivyofanya".


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla akizungumza na Wanachama pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo katika Ukumbi wa Ubungo Plaza , leo NOV 05, 2024.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Moka wa Dar Es Salaam Nag. Abasi Mtemvu, akizungumza na Wanachama pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo katika Ukumbi wa Ubungo Plaza , leo NOV 05, 2024.

Hamasa ya Wanachama pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo katika Ukumbi wa Ubungo Plaza , leo NOV 05, 2024.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages