LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 5, 2024

ZIARA YA DK. NCHIMBI KUTIKISA MIKOA YA SIMIYU, SHINYANGA

 

Na Richard Mwaikenda, Dodoma


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi, Dk. Emmanuel Nchimbi anatarajia kuanza ziara ya siku 6 katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga.

Katika ziara hiyo ya kikazi inayoanza kesho Jumapili, DK. Nchimbi ataanbatana na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid.

Ziara yake itaanza Oktoba 6 katika Mkoa wa Simiyu na kumalizia Shinyanga Oktoba 11, 2024 (kama ratiba Inavyoonesha).

Ziara hiyo ina lengo la kuimarisha uhai wa Chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024.

Katibu Mkuu wa CCM, Balozi, Dk. Emmanuel Nchimbi.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages