LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 23, 2024

TAASISI ZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ZAJIELEZA MBELE YA KAMATI YA BUNGE

Meneja Tehama, Msimamizi wa Kituo cha Kutangaza Utalii Kidijitali cha Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Rossana Mduma  akiwasilisha taarifa ya utendaji na  mafanikio ya kituo hicho katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kilichofanyika katika moja ya kumbi ndogo za Bumbe jijini Dodoma Oktoba 23, 2024.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Pindi Chana akisema neno la utangulizi pamoja na kuwatambulisha viongozi wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo zilizofika kutoa taarifa zao za utendaji katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk.Hassan Abbas. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Timotheo Mzava.

 Taasisi zilizowasilisha taarizaoni; Kituo cha Utangazaji Utalii Kidijitali cha Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Taifa cha Utalii  na Idara ya Malikale.

Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Ephraem Mafulu akijitambulisha katika kamati hiyo.


Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), anayehusika na Taaluma, Tafiti na Ushauri, JescaWilliam akiwasilisha taarifa ya utendaji, mafanikio na changamoto zinzokikabili chuo hicho.
Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika kikao hicho.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mzava (kushoto) akiwa na maafisa wakiweka sawa mambo kabla ya kuanza kikao.
Baadhi ya maafisa wa wiazara hiyo na maafisa wa taasisi hizo.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MHARIRI

BLOG YA TAIFA YA CCM

0754264203


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages