LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 6, 2024

SIMIYU IMEITIKA MKUTANO WA DK. NCHIMBI

sana,” alisema Balozi Dkt. Nchimbi huku akiitikiwa kwa shangwe na vigelegele.


Aidha, Balozi Nchimbi amewaambia wananchi wa Simiyu kuwa Dkt. Samia alivyopokea dhamana ya kuongoza nchi, wapo waliokuwa hawakuamini kuwa miradi iliyoachwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, hasa ile mikubwa ya kimkakati, ingekamilika. Lakini kwa sasa kila Mtanzania ni shahidi kuwa miradi yote inaendelea vizuri katika hatua mbalimbali na mingine imekamilika na inatumika.


Balozi Nchimbi pia amewaambia wananchi kuwa adhabu sahihi ya wanasiasa waliofilisika kisera na hoja, wanaohamasisha vurugu katika jamii kwa siasa za udini, ukabila, ukanda na kuchoma moto vitu, ni kuwanyima kura na kuipigia kura nyingi CCM.


Balozi Nchimbi pia amesisitiza wananchi kuwa mstari wa mbele kwenye kulinda amani ya nchi yetu, na inapotokea mtu yeyote anayetaka kuvuruga amani, akemewe kwa ‘macho makavu’ usoni na akataliwe bila kumuonea haya.


Balozi Nchimbi yupo mkoani Simiyu ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo, akitarajiwa kufanya ziara kwa siku tatu kabla ya kuelekea Mkoa wa Shinyanga, akiwa ameongozana na Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndugu Amos Makalla, pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid.



 Wananchi wakishangilia wakati.Dk. Nchimbi akihutubia katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages