LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 8, 2024

MBIO ZA SEPESHA RUSHWA ZAJA NA ACHA RUSHWA YA NGONO

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mbio za Sepasha Rushwa 2024 zenye Kauli Mbiu ya Acha Rushwa ya Ngono  zitakazofanyika Desemba Mosi jijini Dodoma.

 Shekimweri ameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuziunga kwa asilimia kubwa mbio hizo wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini Dodoma Oktoba 7, 2024.

Kushoto ni Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma,Eugenius Hazinamwisho na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mabalozi wa Sauti ya Wapinga Rushwa (ACVF), Dk. Dinnah Mmbaga. 
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma,Eugenius Hazinamwisho akielezea kufurahishwa na mbio hizo zinazosaidia kutoa elimu ya kupiga vita Rushwa ya Ngono.


Mratibu wa mbio hizo, Eliasa Hussein akitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Shekimweri kwa kuzilea mbio hizo tangu zilipoanzishwa mwaka 2022. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mabalozi wa Sauti ya Wapinga Rushwa (ACVF), Dk. Dinnah Mmbaga akielezea jinsi Rushwa ya Ngono inavyoenea katika Taasisi na. Shule na vyuoni.
Baadhi ya maafisa wa TAKUKURU waliohudhuria mkutano huo. 
Mlezi wa Taasisi ya Mabalozi wa Sauti ya Wapinga Rushwa (ACVF), Otieno Rhera akielezea jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi ya kusaidia kutoa elimu ya kupinga rushwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo hata kwenye michezo kwa kuandaa mbio hizo za Sepesha Rushwa.
 

Baadhi ya wanahabari na mabalozi wa ACVF.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages