Wananchi wa Kata ya Mwandoya, Jimbo la Kisesa, Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, alipokuwa akizungumzia masuala na hoja mbalimbali kutoka kwa wawakilishi wao, Ndugu Basu Kayungilo, Diwani wa Kata ya Mwandoya na Ndugu Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa, leo tarehe 7 Oktoba 2024. Balozi Nchimbi alisimama Mwandoya kuwasalimia wakazi wa eneo hilo na kuzungumza nao masuala ya maendeleo yanayohusu jimbo hilo la Kisesa, akiwa njiani kuelekea Mwanhuzi, Meatu, ambapo ni mwendelezo wa ziara yake ya siku 3, mkoani humo
Mbunge wa Kihesa, Luhaga Mpina akitoa salamu. Kulia ni Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla.
Dk. Nchimbi akisikiliza kero za wananchi na hatimaye kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla akitoa maneno ya utangulizi akijiandaa kumkaribisha Dk. Nchimbi kuzungumza na wananchi.
Wananchi wakishangilia.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇