LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 11, 2024

KANISA HALISI WASHEREHEKEA LANGO KUU LA MWAKA HALISI WA MUUMBA JUU YA NCHI, BABA HALISI ASEMA KUANZIA SASA MIAKA HAITABADILIKA TENA

Kanisa Halisi juzi walifanya Ibada kubwa iliyojaa shamrashamraza aina yake kusheherekea Lango Kuu la mwaka Halisi wa Muumba juu ya Nchi.

Ibada hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, iliongozwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Baba Halisi, na kuhudhuriwa na mamia ya Uzao, Watekeleza Sauti na wa watu kutoka nje ya Kanisa hilo. 

Akihubiri kwenye Ibada hiyo Baba Halisi alisema yafuatayo;

 "Kuanzia sasa miaka haitabadilika tena( ISAYA  66:22-23).


"Kulikuwa na mfumo wa miaka kubadilika badilika kila baada ya vizazi kupita ndio maana baada ya yesu kuzaliwa tulifundishwa kuwa kulikuwa na before Christ na after christ haina maana kabla ya hapo hapakuwa na miaka ilikuwepo ila mfumo ulikuwa unabadilisha badilisha miaka tena kwa kutumia mabaya, ila sasa miaka haitabadilika tena.

1. Kwa mara ya kwanza siku ya kwanza, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza, mwaka wa kwanza ulitokea ( mwanzo 1:1) zilipoumbwa mbigu na nchi. (Yaani 1,1,1,1 ilitokea, ila miaka ilibadilika).

2. Kwa mara ya pili siku ya kwanza, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza, mwaka wa kwanza ilitokea (mwanzo 9:1) baada ya gharika ya nuhu. ( yaani 1,1,1,1 ilitokea ila miaka ilibadilika).

3. Kwa mara ya tatu siku ya kwanza, mwezi wa kwanza, mwaka wa kwanza ilitokea (luka 2:1-6, mathayo 2:1) yesu alipozaliwa wakasema "before christ" na "after christ" ( yaani 1,1,1,1 ilitokea ila miaka iliendelea kubadilika).

4. Kwa mara ya nne siku ya kwanza, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza, mwaka wa kwanza ilitokea Tanzania 28 February 2012(28 Adari 2011) baada ya Adam wa mwisho aliporejesha miezi ya Abibu mpaka Adari kama ilivyokuwa kwa musa katika (kutoka 23:15), (yaani 1,1,1,1 ilitokea ila miaka iliendelea kubadilika).

5. Kwa mara ya tano siku ya kwanza, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza, mwaka wa kwanza ilitokea Tanzania mwaka 2018, Kanisa Halisi tulipotoka kwenye madhabahu ya waliotumwa (yohan 9:7) na kuhamia kwa mkombozi halisi(isaya 59:20), ( yaani 1,1,1,1 ilitokea ila miaka iliendelea kubadilika).

6. Kwa mara ya sita siku ya kwanza, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza, mwaka wa kwanza ilitokea 2020 Muumba alipokuja kwa uhalisia wa moyo safi (mathayo 5:8) ili tumuone, lakini alikuta wengi tuko rohoni ambako kuna magonjwa (rumi 8:23) badala ya kumuona kukatokea ugonjwa wa corona na miaka ikaendelea kubadilika.

7. Ikabidi Ije sauti ya uhai mwaka 2023 ili itutakase na uchafu wote wa roho, nafsi, mwili, asili na mauti (2korintho 7:1) tuliokutwa nao, ambayo imetutakasa kwa mwaka mzima kama (mwanzo 2:1-4) inavyonesha na ilipofika 12 Ethanim, 1 Majira Halisi au (25 August 2024) tulipata siku ya kwanza, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza, mwaka wa kwanza kwa mara ya saba, wakati huu miaka haitabadilika tena unabaki mwaka 1 halisi peke yake". Ndio maana leo (juzi) tunasheherekea lango kuu la mwaka halisi wa muumba juu ya Nchi".


Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi akiongoza Ibada kubwa aina yake kusheherekea Lango Kuu la mwaka Halisi wa Muumba juu ya Nchi. Zifuatazo ni npicha zaidi kuhusu Ibada hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages