LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 26, 2024

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA NHC KWA KAZI NZURI YA UJENZI WA MAJENGO YA SERIKALI MTUMBA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Vuma Augustino ameelezea jinsi wajumbe wa kamati hiyo walivyoridhishwa na kasi ya ujenzi ya majengo nane ya ofisi za serikali unaofanywa na S‏hirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa kiserikali wa Mtumba Makao Makuu ya Nchi Dodoma.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari baada wajumbe wa kamati hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi huo Oktoba 26, 2024..


Mwenyekiti wa kamati hiyo, Augustino (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mary Masanja wakiwaongoza wajumbe kutembelea miradi hiyo.

Wakiendelea  kukagua miradi hiyo.
Moja ya viyoyozi vilivyowekwa katika majengo hayo ambayo ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 87.
Wakiingia kwenye lift zilizowekwa kwenye majengo hayo.
Wakiendelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo


 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages