LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 22, 2024

KAMATI YA BUNGE YA LAAC YAFURAHISHWA NA UFANISI WA MIFUMO YA TAMISEMI

Mkurugenzi wa Tehama wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Erick Kitale akiwapatia uelewa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu mafanikio ya mifumo ya kielektroniki ya wizara hiyo.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Halima Mdee akiendesha kikao cha kupewa uelewa juu ya mafanikio ya mifumo mbalimbali ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Tehama, Erick Kitale katika moja ya kumbi za mikutano za Bunge Jijini Dodoma Oktoba 22, 2024. 

Mdee ameitaka Tamisemi kuboresha zaidi baadhi ya mifumo hiyo ili iendane na wakati uliopo.

Kitale akielezea jinsi mifumo hiyo inavyofanya kazi kwa mafanikio.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stanslaus Mabula akiuliza maswali na kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha zaidi mifumo hiyo.

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Dk. Festo Ndugange akisikiliza kwa makini maswali na ushauri wa wabunge.

Mbunge wa Lulindi ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo, Issa Mchungahela akiuliza maswali.
Mbunge wa Iringa Mjini, Dk. Jesca Msambatavangu.
Mbunge wa Kondoa Mjini Ally Makoa.


 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages