Na Mwandishi Wetu, Tanga Mjini
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amewataka wanawake wote nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali bila kuogopa lolote lile.
Aidha, Chatanda amewataka wanaume wote kuendelea kuwaunga mkono wanawake wenye karama na uwezo mkubwa wa uongozi na bila ubaguzi wowote ule.
Aidha, amehimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa ajili ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024. Uandikishaji untamatika leo.
Ameyasme hayo alipotinga mitaani mjini Tanga kuhamasissha wananchi kwenda kujiandikisha katika daftari hilo.
Chatanda akizungumza na mmoja wa akina mama kwa lengo la kumhamasissha kwenda kujiandikisha. Nyuma yake ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇