Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi kesho, 5 Kisleu 1 Majira Halisi (Oktoba 13, 2024) atafanya mkutano mkubwa wa kihistoria na wananchi wa Manispaa ya Kigoma - Ujiji kufafanua kwa kina Sauti Kuu ambayo aliisikia Bustani Halisi, Kigoma, Tanzania, mwaka 2015, 2019, 2020 na 2023.
Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta, Namanga jijini Dar es Salaam, imesema mkutano huo utafanyika Mwanga Community Centre, kuanzia saa 8 mchana hadi saa 10 jioni na kuomba kila mmoja asikose nafasi hiyo.
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇