LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 16, 2024

BABA HALISI AFAFANUA KIGOMA: SAUTI NILIYOPEWA SIYO YA KIDINI AU YA MTU BINAFSI ANAYETAFUTA UMAARUFU, TUSIGOMBANE, TUSITOANE NGEU, NI YETU SOTE

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Kigoma-Ujiji

Kwa mujibu wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi,  Alfajiri ya saa 9 hadi saa 11 lango la kuamkia 27 Buli, 1 Majira Halisi (7 Oktoba 2024), Sauti ya Muumba ilikuja akiwa sebuleni kuwa afike Manispaa ya Kigoma - Ujiji kufafanua jinsi alivyoisikia Sauti Kuu ya Muumba wa Vyote, Wote na Yote Mwaka 2015, 2019, 2020 na 2023.


Bila shaka, Sauti hiyo ya Muumba ilimuagiza hivyo Baba Halisi, baada ya kuonekana kuwa kulikuwa kuna baadhi ambao walikuwa bado hawajapokea kwa upendo Sauti Kuu aliyopokea katika miaka hiyo tajwa.


Katika kutekeleza, Kanisa Halisi liliandaa mkutano mkubwa wa Kijamii ambao ulifanyika 5 Kisleu, 1 Majira Halisi sawa na Oktoba 13, 2024, katika Uwanja maarufu wa Mwanga Community Centre,  Manispaa ya Kigoma - Ujiji.


Mkutano huo ulianza saa 8 hadi saa 10 jioni, ukifunguliwa na Genoveva Samwel Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kisangani, Kata ya Mwanga Kaskani, ambako ndilo lililopo eneo la Mwanga Community Centre ulikofanyika mkutano.


Mkutano ulifunikwa na amani na utulivu bila ubaguzi, huku waliohudhuria wakiwa wachangamfu, wakicheza na kufurahi muda wote, wakiwemo Watekeleza Sauti kutoka mikoa zaidi ya kumi, Uzao wa Kanisa Halisi mkoa wa Kigoma na mikoa jirani, viongozi mbalimbali wa Serikali vyama vya siasa na viongozi na waumini wa dini na madhehebu mbalimbali.


Baada ya burudani ya nyimbo za kumtukuza Muumba, ukafika wakati wa Hotuba rasmi ya Baba Halisi kufafanua alivyoisikia Sauti Kuu ya Muumba 2015; 2019; 2020 na 2023.


Kwa kuwa Baba Halisi hakuwepo mubashara lakini akawepo kwa sauti yake, Hotuba ilisomwa kwa umahiri mkubwa na Mtekeleza Sauti Mwandamizi Amani Halisi kutoka Makao Makuu ya Kanisa Halisi, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, kama ilivyoandikwa na Baba Halisi mwenyewe.


Katika Hotuba hiyo Baba Halisi alisema mengi makubwa ikiwemo kusisitiza akisema;  "Sauti Kuu niliyopewa sio ya kidini wala ya kidhehebu au ya Huduma binafsi, kama baadhi wanavyodhani! Ni kwa faida ya wote, bila kujali dini, dhehebu au mtu yeyote.


Tusigombane; tusipigane; tusitoane ngeu. Sauti hii ni yetu sote, siyo ya mtu mmoja tu anayetafuta umaarufu, hapana. Ni yetu sote".

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi.

Hotuba kamili ya Baba Halisi, Kigoma hii hapa.👇


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages