LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 25, 2024

RAIS SAMIA AZINDUA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa wakifunua pazia jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa  Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, leo tarehe 25 Septemba 2024, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma.

Rais Samia akikata utepe wakati wa uzinduzi wa jengo hilo. Kutoka kushoto ni Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa wa Ruvuma, Oddo Mwisho na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa CCM, Dk. Frank Hawassi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa eneo la Kigonsera, Wilaya ya Mbinga, baada ya kuzindua jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, leo tarehe 25 Septemba 2024, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma.



Muonekano wa jengo lililozinduliwa.


Wananchi wakiwa na furaha.
Sehemu ya umati wa wananchi ulihudhuria uzinduzi huo.



 



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages