LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 25, 2024

RAIS SAMIA APATA UHAKIKA WA UHIFADHI SALAMA WA MAHINDI NFRA MBINGA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 25 Septemba 2024, alipata maelezo kuhusu usafishaji na upimaji wa mahindi unaofanywa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) katika kituo cha ununuzi wa mahindi kilichoko eneo la Soko Kuu, Mbinga mjini, kabla ya kuwasalimu na kuzungumza na wananchi wengi waliokusanyika kumlaki na kumsikiliza.


Kutokana na maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia, katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, NFRA imeweka vituo kwa ajili ya kununulia mahindi ya wakulima katika maeneo mbalimbali nchini, hususan katika mikoa inayozalisha mazao hayo kwa wingi. Hatua hii, mbali na kuwahakikishia wakulima soko la uhakika la mahindi yao na kuwapunguzia adha ya kuyasafirisha umbali mrefu, pia inawalinda dhidi ya ulanguzi wa wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu. Aidha, ni mojawapo ya mipango ya Serikali kuweka utaratibu mzuri wa kuyafikisha mahindi hayo katika soko la kimataifa kwa ajili ya manufaa ya wakulima na taifa kwa ujumla.

Rais Samia akiangalia mahidi alipokuwa akipata maelezo kuhusu usafirishaji na upimaji wa mahindi katika moja ya maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) katika kituo cha ununuzi wa mahindi kilichoko eneo la Soko Kuu, Mbinga mjini.






 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages