Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na
kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping katika ukumbi wa
The Great Hall of the People.
Katika mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia amesema uhusiano wa nchi hizo mbili ni muhimu na
ametoa wito wa kuendelea kudumisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali pamoja na
kuendeleza ushirikiano katika Mpango wa Kuendeleza Miundombinu na Kukuza Uwekezaji (Belt
and Road Initiative) ili kuleta manufaa yanayoonekana kwa wananchi.
Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa sekta binafsi nchini China kuwekeza Tanzania katika uzalishaji
wa vyanzo vya nishati mbadala na miundombinu ya usambazaji.
Katika mkutano huo, Rais Xi alisema kuwa China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kimkakati
kati yake na Tanzania ili kuleta manufaa zaidi kwa nchi zote mbili na kuendeleza uhusiano wa
kihistoria ulioasisiwa na waasisi na kurithiwa na vizazi vya sasa.
Rais Xi pia amesema China inaiona Tanzania kuwa ni mfano mzuri wa mahusiano kati ya nchi
zinazoendelea katika muktadha wa ushirikiano wa China na nchi za Afrika.
China na Tanzania zimekubaliana kuendelea kubadilishana uzoefu na kupeana mafunzo katika
maeneo mbalimbali ya kiserikali.
Akizungumzia kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati
ya China na Afrika (FOCAC), Rais Samia ameeleza imani yake kuwa mkutano huo utakuwa na
mchango mpya katika kuimarisha ushirikiano wa kirafiki kati ya Afrika na China na kuhamasisha
mchakato wa viwanda na kilimo cha kisasa barani Afrika.
Baada ya mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia, Rais Xi Jinping na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde
Hichilema walishuhudia uwekaji saini wa Hati ya Makubaliano (MOU) baina ya Tanzania,
Zambia na China kuhusu uboreshaji wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa
Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China (CPPCC), Mhe. Wang
Huning
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇