LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 14, 2024

MUSSA KILAKALA : TUULINDE MUUNGANO WETU KWA WIVU MKUBWA

 NA VICTOR MAKINDA. MOROGORO

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro, Mussa Kilakala amewataka  Watanzania bara na visiwani kuulinda Muungano kwa wivu mkubwa na kuwashughulikia haraka watu wote wenye malengo ovu ya kuteteresha misingi ya Muungano wetu.

Kilakala  ameyasema hayo mjini Morogoro leo, wakati alipokuwa akizungumza na taasisi ya Vijana Nguvukazi kutoka Kizimkazi  Zanzibar, waliwasili mkoani hapa kwa ziara ya siku 3.
 
Alisema kuwa manufaa yatokanayo na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni makubwa hivyo ni lazima Muungano huo ulindwe kwa wivu mkubwa.

 "Manufaa ya kisiasa, kiuchumi na kiulinzi yanayotokana  na Muungano wa Tanganyika  na Zanzibar ni makubwa na yenye tija, hivyo ni lazima tuulinde Muungano wetu ili tuendelee kunufaika nao.

 Kilakala aliwataka vijana hao kutika taasisi ya  vijana nguvu  kazi kuhakikisha kuwa wanaendelea kuhubiri faida za muungano mahamu popote.
 
 
Akizungumza  mara baada ya kuwasili mkoani hapa, Katibu mtendaji wa taasisi ya Vijana nguvu kazi,  Abuu Juma,  amesema ziara hiyo imepewa jina la Muungano Tour, wameifanya kufuatia mwaliko wa Taasisi ya Walimu Wazalendo ya wilayani  Kilombero huku lengo kubwa likiwa ni kuendelea kuimarisha Muungano na udugu baina ya watu wa Tanzania bara na Viwani.
 
 "Ziara yetu tumeipa la Muungano Tour ikiwa na lengo kuu la kuja kuangalia vivutio  vya utalii vilivyopo mkoani Morogoro, kuimarisha Mungano na kuhamasisha wananchi ushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika  Novemba  mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya  ya Morogoro, Mussa Kilakala, akizungumza na  vijana wa Taasisi ya Vijana Nguvukazi  kutoka kijiji cha Kizimkazi Zanzibar wakati walipowasili mjini Morogoro

 

 


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages