LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 14, 2024

DC MPOGOLO AWATULIZA KIPUNGUNI, MALIPO YA FIDIA KUANZA MWEZI UJAO, RAIS DK. SAMIA AMESHATOA MAELELEKEZO

Ilala, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, amesema Rais Dk. Samia Suluhu  Hassan, ameshaelekeza  wananchi
wa Mtaa wa Kipunguni Kata ya Kipawa, waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerer (JNIA) waanze kulipwa fidia zao.


DC Mpogolo ameyasema hayo jana, katika mkutano wa hadhara wa  kusikiliza na kutatua kero za wanchi wa Kata za Minazi Mirefu, Kiwalani na Kipawa.

“Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameshatoa maelekezo kwamba malipo yaanze kufanyika hivyo kinachosubiriwa  hivi sasa ni mifumo ya namna gani malipo yaanze kufanyika,”alisema Mpogolo.

Aliwahakikishia wananchi hao wa Kipunguni wataanza kulipwa ndani ya Oktoba mwaka huu, na kuagiza siku ya Jumanne, Septemba 17, 2024, saa 2:00 asubuhi viongozi wa kamati wafike ofisini kwake ili wapate uhakika halafu kisha wakawaambie wananchi, kauli ambayo ilifanya mkutano kulipuka kwa shangwe huku wananchi wakiimba wimbo wa "Tuna imani  na Samia, Oyaa! Oyaa! Oyaa''.

 

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages