Na CCM Official Blog, Magomeni
Viongozi, Watendaji wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana, walifanya kikaokazi kikubwa kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mafanikio ya utekelezaji miradi mbalimbali, lengo likiwa ni kutaka mafanikio hayo yajulikane kinaga ubaga hadi ngazi za chini.
Kikao hicho kilihuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Saad Mtambule, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Shaweji Abdallah na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James ambaye alialikwa maalum kwa ajili ya kutoa mada kuhusu umuhimu wa viongozi, watumishi na Watendaji wa serikali na Chama kuzingatia mawasiliano na mahusiano na wananchi.
Kikaokazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Soko la Kisasa la Magomeni, kilihudhuriwa pia na Makatibu wa CCM na Watendaji wa serikali kutoka Kata zoteMkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akizungumza kwenye kikaokazi hicho.
DC Mtambule akiongoza viongozi kuingia ukumbini.
Viongozi wakiwa wamesimama kuimba wimbo wa taifa na wa Afrika Mashariki mwanzoni mwa kikao kazi hicho. Baadhi kutoka kushoto ni DC Kheri James, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Sahweji Abdallah, DC Mtambule na Mstahiki Meya Songoro Mnyonge.
Watendaji mbalimbali wakiwa wamesimama kuimba nyimbo hizo.
Mwenyekiti wa CCM Kinondoni Abdallah Shaweji akiteta jambo na DC Mtambule kabla ya kikaokazi hicho kuanza.
Washiriki wakiwa kwenye kikaokazi hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikaokazi hicho.Washiriki wakiwa kwenye kikaokazi hicho.Washiriki wakiwa kwenye kikaokazi hicho.DC Mtabule akifungua kikaokazi hicho.
DC Mtabule akiendelea kuzumzia umaalum wa kikaokazi hicho.DC James akitoa mada ya uhusiano na mahusiano baina ya viongozi, watendaji na watumishi kwa wananchi.
DC Mtambule akimpongeza DC James baada ya mada.
Washiriki wakimshangilia DC Mtambule aliposema ''Rais Dk. Samia Mitano tena''
DC Mtambule akizungumza na kusema "Rais Dk. Samia Mitano tena".
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Abdallah Shaweji akizungumza katika kikao kazi hicho. Alizungumzia haja ya viongozi wa CCM na wa Serikali kujiandaa vilivyo ili kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika vizuri huku akisisitiza viongozi wa CCM kuhakikisha Chama kinaibuka na ushindi wa kishondo kwenye uchaguzi huo.
Your Ad Spot
Sep 5, 2024
KIKAOKAZI CHA VIONGOZI WA SERIKALI NA CCM WILAYA YA KINONDONI KILIVYOFANA
Tags
featured#
Home#
Share This
About Bashir Nkoromo
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇