LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 5, 2024

DKT SAMIA AMEFANYA MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA ELIMU - CPA MAKALLA







đź’  _Shule za High School zilikuwa chache lakini leo zipo kila Mkoa, Miongoni mwao za Wasichana zikiwa na Michepuo ya Sayansi_


Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla leo Septemba 05, 2024 amekagua Ujenzi katika Sekondari ya Samia ya Wasichana Mchepuo wa Sayansi iliyopo Wilayani Longido Mkoani Arusha.


CPA. Makalla akiambatana na Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) amezungumza na Wanafunzi na Walimu kwenye Sekondari hiyo, ambapo amesema Rais na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt Samia Suluhu Hassan amefanikiwa kuleta mapinduzi Makubwa Kwenye Sekta ya Elimu hapa nchini.


"Nataka niwaambie kitu kimoja kuwa, tumefika hapa kwa Sababu enzi hizo nasi tulisoma kama Ninyi, kwa hiyo mnapaswa kuongeza Jitihada kwenye masomo ili nanyi muwe Viongozi Bora kwa Siku zinazokuja"


"Pongezi nyingi zimuendee Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Elimu, kwa Sababu Zamani high school zilikuwa Chache, lakini Rais Dkt Samia amefanya mapinduzi kwenye Elimu, ambapo kwa Sasa Kila Mkoa unayo shule ya Mfano ya Wasichana Mchepuo wa Sayansi, hayo ni maono yake na Sisi kama Chama hatuna budi kupongeza na kuunga mkono Jitihada zake" amesema CPA. Makalla. 



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages