LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 17, 2024

KIGAHE AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI RUSUMO

 

Meneja wa kituo Cha forodha cha Rusumo upande wa Tanzania Bw. Amosi Illoyo (mwenye Shati la bluu) akielezea kazi mbalimbali zinazofanywa na mpakani hapo upande wa Tanzania Mhe. Naibu Waziri wa Viwanda (Mwenye Shati jeupe) na Biashara alizotembelea kituo hicho Ili kuona shughuli za kibiashara katika mpaka huo.

…..

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ( Mb)amefurahishwa na utendaji kazi wa wafanayakazi katika mpaka wa Rusumo.

Mhe. Kigahe ameyasema hayo alipofanya ziara ya kutemebelea mpaka wa Tanzania na Rwanda ( Rusumo ) kwa lengo kuangalia shughuri za Biashara zinazofanyika katika mpaka huo.

Akiongea wakati wa kujibu taarifa ya utendaji wa kituo hicho kutoka kwa Meneja wa kituo hicho ,Mhe Kigahe amefurahishwa na utendaji wa kituo hicho kwa uchapakazi,uadilifu na kujituma kwa watumishi.

“Nimefurahishwa na taarifa ya kutumia muda machache wa kuvusha magari na watu kwa kutumia dk 32 tofauti na upande wa pili wanaotumia muda mwingi” ,Amesema Kigahe.

Aidha amesisitiza kuwa soko la kimkakati la Kahaza linalojengwa litakapoanza kutumika lisaidie wakulima kukusanya mazao toka shambani na kuweka lebo kwenye vufungashio ili kuipa thamani bidhaa yetu kutambulika kitaifa na Kimataifa.

Kwa upande wake Meneja wa kituo Cha forodha cha Rusumo Amos Illoyo amemshukuru Naibu Waziri kwa kufanya ziara kituoni hapo na kuona shughuri za kibiashara zinavyofanyika.

Ameeleza kuwa Shughuli zinazofanyika katika mpaka huo ni kukusanya mapato ya serikali ,kuthibiti biashara za magendo zinazofanywa maeneo yanayozunguka mpaka ili kuwezesha ulipaji kodi,na kuzuia bidhaa bandia.

Mpaka wa Tanzania umekuwa ni lango kuu la kupitisha bidhaa kwenda nchi za Rwanda na Congo Drc.huku bidhaa zinazopita kwa wingi zikiwa Cement , vinywaji baridi.

Nae Afisa Biashara wa wilaya ya Ngara Bw. Privanus Katinhila amesema kuwa kupitia ziara ya Naibu waziri amejifunza mengi ikiwemo maelekezo aliyopewa ya kujikita kutoa Elimu kwa wafanyabiashara ili kazi yake ifanyike kwa weledi.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (katikati) Kaimu DAS Wilaya ya Ngara Jawali Yusufu (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe.Ndaisaba Ruhoro(Kulia ) Wakiwa katika kikao Cha kupokea taarifa ya utendaji kituo Cha forodha upande Tanzania Rusumo  katika ukumbi wa Ofisi za kituo Cha forodha Rusumo.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mwenye Shati jeupe ) akisalimiana na OCD wa Wilaya ya Ngara William Sola mara baada ya kuwasili katika kituo Cha forodha cha Tanzania upande wa Tanzania kuangalia shughuri za Biashara zinazoendeshwa katika kituo hicho. Aliyesimama katikati mwenye Shati ya bluu ni Meneja wa kituo Cha forodha Bw. Amosi Illoyo.

Meneja wa kituo Cha forodha cha Rusumo upande wa Tanzania Bw. Amosi Illoyo (mwenye Shati la bluu) akielezea kazi mbalimbali zinazofanywa na mpakani hapo upande wa Tanzania Mhe. Naibu Waziri wa Viwanda (Mwenye Shati jeupe) na Biashara alizotembelea kituo hicho Ili kuona shughuli za kibiashara katika mpaka huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages