
Wananchi Kijiji cha Kamunazi wilayani Ngara, Kagera, wakiwa na furaha kumsikia Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akijibu kupitia simu aliyompigia Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi akimuagiza aende kijijini hapo kutatua kero ya maji.
DK. Nchimbi ametoa utatuzi huo msafara wake uliposimamishwa na wananchi wa eneo hilo na kutoa kero ya maji na umeme smba umefika kwa kuwasha transfoma lakini bila kuwaunganishia wananchi.
Msafara wake ulikuwa unatoka Biharamulo kwenda Ngara kuwahi kuhutubia mkutano wa hadhara.
DK Nchimbi ameanza jana ziara ya kikazi mkoani Kagera, baada ya kumaliza katika Mkoa wa Kigoma.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇