LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 22, 2024

SIYO DHAMBI VIONGOZI WA DINI KUHUDHURIA MIKUTANO YA SIASA-ASKOFU CHANDE

Askofu Mkuu wa Kanisa la Karmeli Assemblies Of God (KAG), Dk. Evance Chande ametoa wito kwa viongozi wa dini kujenga tabia ya kushirikiana na Serikali hata kuhudhuria mikutano ya siasa kwa lengo la kuzijua sera zao na wagombea wazuri watakaoamua kuwapigia kura wakati wa uchaguzi.


Amesisitiza kuwa siyo dhambi kwa viongozi hao na waumini wao kuhimizana kuhudhuria mikutano hiyo kwa lengo la kuyajua mambo hayo muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa.


Pamoja na mambo mengine Askofu Dk. Chande ameyasema hayo wakati wa semina elekezi kwa wachungaji wa kanisa hilo lililopo Ipagala Makao Makuu ya Nchi Dodoma Agosti 22, 2024.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages