LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 21, 2024

RAIS SAMIA ANAKESHA KUWAHANGAIKIA WATANZANIA- KOMREDI RABIA


 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye ni Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid akielezea jinsi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anavyokesha kufanya kazi akihangaikia maisha ya Watanzania.

Rabia ambaye ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati Kuu walioambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara mkoani Geita Agosti 13, 2024. Wajumbe wengine ni Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Ussi Haji (Gavu). Dk Nchimbi alihitimisha ziara yake hiyo mkoani Mwanza Agosti 15, 2024, aliyoifanya katika mikoa mingine mitatu ya Kigoma, Kagera, Geita. Tangu ashike wadhifa huo, ameshafanya ziara katika mikoa mingine 13 ambayo ni; Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Lindi na Mtwara. Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI 
BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages