LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 31, 2024

RAIS DK. SAMIA ASHUHUDIA MASHINDANI YA KIMATAIFA YA QUR AN, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, ameshuhudia Mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa,  jijini Dar es Salaam.


Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa haki, amani, kuheshimiana, na kustahimiliana kama nguzo za kuimarisha umoja wetu kama taifa. 


Ameeleza kuwa mashindano haya yanachangia katika kuimarisha maadili ya kitaifa na kudumisha mshikamano miongoni mwa wananchi wa Tanzania bila kujali tofauti za kidini au kikabila.


Rais Samia pia amegusia umuhimu wa kuendeleza familia na maadili ya nchi, akibainisha kuwa familia yenye misingi imara ni msingi wa taifa lenye nguvu.


Amehimiza wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa katika mazingira ya heshima, amani, na upendo ili kuijenga jamii yenye maadili bora.


Pia Rais Samia ameweka mkazo juu ya nafasi ya mwanamke katika jamii, akisema  mwanamke ni mhimili wa familia na jamii kwa ujumla. 


Amepongeza wanawake kwa kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto na kujenga maadili ya familia na kukumbusha kuwa mtoto wa kiume naye asisahaulike katika malezi na miongozo ya maadili, kwani watoto wote wanapaswa kulelewa kwa usawa ili kuwa na jamii yenye uwiano.


Mashindano haya ya Qur'aan yameleta pamoja washiriki kutoka mataifa mbalimbali, yakiwa ni jukwaa muhimu la kukuza maadili, uelewano, na mshikamano wa kimataifa. 


Rais Samia amewapongeza washiriki wote na kuwatakia kila la heri katika mashindano hayo, akisisitiza kuwa washindi ni wale wote waliohudhuria na kushiriki kwa dhati.


Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kudumisha amani, mshikamano, na maadili mema ili kuhakikisha kuwa Tanzania inabaki kuwa kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa duniani.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages