LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 27, 2024

RAIS DK. SAMIA AHUDHURIA UZINDUZI WA KAMPENI YA ODINGA, KUWANIA UENYEKITI KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA (AU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mwenyeji wake Mhe. Dkt. William Samoei Ruto, Rais wa Jamhuri ya Kenya katika Ikulu ya Nairobi tayari kwa kuhudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), tarehe 27 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Mhe. Dkt. William Ruto Rais wa Jamhuri ya Kenya pamoja na Viongozi wengine wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Ikulu ya Nairobi, tarehe 27 Agosti, 2024. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwa ni mualiko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Dkt. William Samoei Ruto, Ikulu ya Nairobi, tarehe 27 Agosti, 2024.

Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni  ya Umoja wa Afrika (AU) akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni , Ikulu ya Nairobi, tarehe 27 Agosti, 2024. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mhe. Dkt. William Samoei Ruto Rais wa Jamhuri ya Kenya pamoja na Viongozi wengine wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Ikulu ya Nairobi, tarehe 27 Agosti, 2024.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages