LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 27, 2024

MGONJWA ALIYELAZWA MUHIMBILI AMTOA MACHOZI NAIBU MEYA URIO, RAIS DK. SAMIA, JAMII WAOMBWA KUSAIDIA MATIBABU

Na Bashir Nkoromo, CCM Official Blog
Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Michael Urio ametokwa machozi ya huzuni baada ya kumuona kijana Karume Ali Karume alivyokosa tabasamu kutokana na maradhi ya kuvimba nyama sehemu kadhaa za mwili, yanayomsibu.

Urio ambaye ni Diwani Kata ya Kunduchi, ametokwa machozi hayo leo Agosti 27, 2024, alilpoenda kumjulia hali Karume katika Wodi ya Kibasila, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa, tangu Agosti 24, 2024.

Akizungumza baada ya kutoka wodini, Urio  amesema kwa hali aliyoshuhudia ugonjwa na kuelezwa hali ya kiumi ya familia ya mgonjwa, unahitajika msaada ili Karume apate matibabu maana hana uwezo wa kugharamia matibabu ambayo kulingana na ugonjwa ulivyo itakuwa ya mamilioni ya fedha.

"Baada ya kumuona na kuzungumza naye nimeona kwa kweli ugonjwa alionao kijana huyu ni mkubwa, umemnyima kabisa tabasam.

Kwa hali ile unahitajika msaada wa sisi sote, Rais wetu na Mama yetu Dk. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri, Wabunge na kila mwenye kuweza kufanya chochote ili kijana huyu apate matibabu na kurejeshewa tabasam", akasema Urio.

Mkurugenzi wa Huduma ya Upasuaji Muhimbili Dk. Rachel Mhavile naye alisema, baada ya kumpokea Karume wamemfanyia vipimo vya kujua ugonjwa unaosibu na pia namna upasuaji utakavyofanyika.

"Karume tulimpokea Jumamosi. Kwa kweli kijana huyu anaumwa. Tumeshamfanyia vipimo kujua ugonjwa gani unaohusika, na pia kujua namna gani tutamfanyia upasuaji ikiwemo gharama.

Sasa tunasubiri majibu ya vipimo. Hatujaanza kumpatia matibabu lakini kwa maumivu anayopata tumekuwa tukimpa dawa za kutuliza maumivu tu", akasema Dk. Rachel ambaye alisema amezungumza mbele ya Naibu Meya Urio, kwa niamba ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili Mohamed Janabi.

Salum Hidobelele, alisema Karume ambaye ni mpwa wake, ameungua ugonjwa alionao kwa takriban miaka 20 sasa, lakini hawakuweza kumpeleka hospitali kwa kuhofia uwezo mdogo walionao kuweza kumudu gharama za mtibabu hivyo akaendelea kumuuguza nyumbani kwake Mbagala Kilungule.

Safari ya Karume hadi kufika Muhimbili imetokea naada ya Wanachama wa Club ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam, kupata taarifa, na walipomuona kuwa na hali mbaya walimpeleka Hospitali ya mkoa wa Temeke ambayo nayo ilimhamishia Muhimbili.

Naibu Meya ya Manispaa ya Kinondoni ambaye ni Diwani wa Kunduchi Michael Urio akimjulia hali Katume Ali Karume katika wodi ya Kibasila, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, leo Agosti 27, 2024. Kulia ni Mjomba wa Karume, Salum Hidobelele mkazi wa Mbagala Kilungule.
Naibu Meya Urio akitazama mgonjwa alivyoathirika.
Diwani Urio akizungumza na mgonjwa huyo.
Mkurugenzi wa Huduma ya Upasuaji Muhimbili Dk. Rachel Mhavile, akizungumza baada ya yeye na Naibu Meya Urio (kulia), kutoka wodini kuona mgonjwa.
Naibu Meya Urio, akizungumza baada kutoka wodini kuona mgonjwa.
Naibu Meya Urio akatokwa machozi
Ikabidi Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili  Dk. Rachel Mhavile amtulize.
Mjomba wa Karume (mgonjwa), Salum Hidobelele mkazi wa Mbagala Kilungule akizungumza.
Careen Mgonja, Makamu Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam, kusaidia harakati za mgonjwa Katume kupata matibabu akizungumza.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages