Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akihamasisha wajumbe wa mkutano wa ndani wa viongozi wa CCM Bukoba uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi leo Agosti 10, 2024.
Dk Nchimbi yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku 6 ambapo kabla ya mkoa huo amefanya ziara katika mkoa wa Kigoma. Hadi sasa na timu yake wamefanya ziara katika mikoa 15.
Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Balozi Dk. Nchimbi, kwenye hiyo ziara ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) - Oganaizesheni, Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid.
Komredi Dk Nchimbi (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wengine wakati wa kutoa hamasa katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Ussi Haji (GAVU) kulia, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdallah Hamid na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Karamagi.
Dk Nchimbi akihutubia katika mkutano huo.
Mbunge wa Bukoba Vijijini, Dk. Jasson Rweikiza akiwa na Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Kagera, Mushahu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Karim Amri akisalimia wajumbe wa mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Rabia Abdallah Hamid akitoa somo katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Zainab Katimba akitambulishwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo akitambulishwa.
Aliyehi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CHADEMA, Upendo Peneza akitambulishwa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Nazir Karamagi akizungumza neno la utangulizi akijiandaa kumkaribishaDk Nchimbi kuhutubia katika mkutano huo.
Kada wa CCM, Lydia Mpanju mwenye umri wa miaka 84 akihamasisha kwa kuimba wimbo wa lugha ya kihaya wakati wa mkutano huo. Bibi Mpanju alijiunga na TANU 1958. Amehimiza wana CCM kudumisha mshikamano.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇