Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli alipozuru kaburi hilo Chato, mkoani Geita Agosti 11, 2024.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Chato, amewapongeza wanaChato kwa kuzaa shujaa John Magufuli amaye amelifanyika mambo makubwa Taifa hivyo CCM itaendelea kumuenzi Hayati Magufuli kwa mambo mengi mazuri aliyoyafanya kwa Taifa.
Pia amesema kuwa wanamshukuru Hayati Magufuli kwa kuteua mgombea mwenza Makamu wa Rais wakati huo Samia Suluhu Hassan ambaye sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye anaendeleza miradi yote aliyoianzisha marehemu.
Enzi za uhai wake Hayati Magufuli alikuwa Mbunge wa Chato kwa miaka 20 na ameutumia uwaziri kwa miaka 20 na urais mpaka mauti yalipomkuta.
Dk Nchimbi ameanda ziara ya siku 3 mkoani Geita baada ya kumaliza katika Mkoa wa Kagera.
Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Balozi Dk. Nchimbi, kwenye hiyo ziara ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) - Oganaizesheni, Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla akiweka shada la maua katika kaburi hilo.Katibu wa Oganaizesheni, Issa Ussi Haji (GAVU)
Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Zainab Katimba.
Dk Nchimbi akizungumza baada ya kuweka shada la maua.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇