Moja ya majengo15 ya ofisi za CCM yaliyojengwa kwa msaada wa Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Musukuma katika jimbo hilo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akimpongeza Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma (anyeshangilia) kwa moyo wake wa kujenga kwa gharama zake majengo 15 ya ofisi za CCM katika jimbo hilo. Kila jengo amejenga kwa hgarama ya sh. mil. 30.
Ametoa pongezi hizo aliposimama kuwasalimia wanancji eneo la Kasota na Rwezera jimboni humo akiwa njiani kuelekea Nyehunge Jimbo la Bushosha kuendelea na ziara ya siku mbili mkoani Mwanza. Agosti 14, 2024.
Dk. Nchimbi amewaomba watu wengine wenye nafasi zao kuiga mfano huo wa Musukuma kwa kusaidia kujenga ofisi kama hizo, pia kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ya Taifa.Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Balozi Dk. Nchimbi, kwenye hiyo ziara ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) - Oganaizesheni, Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla
Manaibu Waziri wakiwa tayari kujibu kero mbalimbali zinazotolewa na wananchi. Kutoka kushoto ni Daniel Sillo (Mambao ya Ndani ya Nchi), Zainabu Katimba (TAMISEMI) na Godfrey Kasekenya wa Ujenzi.
Wananchi wakisiliza huku wengine wakishangilia wakati Dk Nchimbi akihutumia katika maeneo hayo.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇