LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 29, 2024

BUGOTA AMSHUKURU RAIS DK. SAMIA KUIPATIA IGUNGA MIRADI TELE



Na HEMEDI MUNGA, Igunga 


MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Lucas Bugota amemshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali wilaya hiyo kwa kuipa miradi mingi ya maendeleo.


Aidha, amesema Rais Dk. Samia ameifanyia wilaya hiyo mambo makubwa ambayo yanawanufaisha wananchi wa wilaya hiyo.


Bugota ametoa pongezi hizo wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kupokea taarifa ya hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 30, 2024, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo mjini hapa.


"Kwa dhati tunamshukuru Rais Dk.  Samia Suluhu Hassan na kumuombea kwa  Mwenyezi Mungu aendelee kumbariki  kwa sababu tumepata miradi kila kona, hakia ametujali sana," ameshukuru.


Katika hatua nyingine, Bugota amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Selwa Abdalla Hamid  kwa usimamizi madhubuti ambao umesaidia kuandaa na kukamilisha  taarifa hiyo.


Amesema hakika wataalam hao wamekua wakiandaa taarifa  kwa umakini, hivyo Halmashauri hiyo kuonekana ikifanya vizuri.


"Nikupongeze  sana Mkurugenzi kwa sababu wataalam wamekua wakifanya vema kwa sababu unawawezesha kwa kila namna," amepongeza.


Mbali na hayo, Bugota amewaomba wataalam hao kuendelea kuchapa kazi kwa sababu baraza hilo linahitaji upendo na kuona Halmashauri inakwenda vizuri muda wote.


Amedokeza kuwa Halmashauri inakwenda vizuri kwa sababu ya uchapa kazi wao hususan katika ukusanyaji wa mapato ambao ameuhimiza  uongezeke.


"Ndugu zangu viongozi ili twende vizuri lazima Halmashauri iwe na mapato ya kutosha kwa lengo la kuhakikisha shughuli zinakwenda na hazikwami," amesisitiza.


Kwa upande wa Mwakalishi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo, Shani Mangesho amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa sababu ya kuwagharamia wataalam wake walioandaa muhutasari (summary) wa taarifa hiyo kwa kuwa sio jambo dogo.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Selwa Abdalla Hamid amemuhakikishia Mwenyekiti huyo kuwa wataendelea kusimamia shughuli za Halmashauri kwa lengo la kuhakikisha inaendelea kupaa.


Rasimu ya Taarifa za mwisho za Hesabu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 zimeandaliwa kwa kuzingatia kanuni ya 31(4), LAAM 2019 ikiwemo matakwa ya mfumo mpya wa viwango vya kimataifa vya Hesabu za Sekta ya Umma.






 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages