Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe katika Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ambacho, mbali ya viongozi wa vyama hivyo, pia kilihudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri wakiwakilisha upande wa Serikali. Mbowe hivi sasa ni Mwenyekiti wa TCD.
Baadhi ya viongozi wakuu wengine wa vyama hivyo walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ndugu Dorothy Semu, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Ndugu Joseph Selasini, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi.
Upande wa Serikali, uliwakilishwa na Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Afya, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Festo Ndugange, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mhe. Daniel Sillo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kikao hicho kimefanyika Jumapili, Agosti 18, 2024, jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇