LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 23, 2024

RAIS DK. SAMIA ATENGUA UTEUZI WA VIGOGO WAANDAMIZI TTCL, POSTA NA UCSAF

Ikulu, Dodoma
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi wa juu kabisa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Posta Tanzania na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Moses Kusiluka aliyoitoa leo, Julai 23, 2024, imetaja waliotenguliwa kuwa ni;

Mwenyekiti wa  Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Zuhura Sinare Muro na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo (TTCL) Mhandisi Peter Rudolph Ulanga.

Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Shirika la Posta Tanzania  Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla mabongo na Posta Masta Mkuu wa Shirika hilo Maharage Ally Chande.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Prof John Nkoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Justina Tumaini Mashiba.

Rais Dk. Samia

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages