Ofisi ya Bunge, Dodoma
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amejiuzulu Ubunge wa kuteuliwa na Rais.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, imesema Mbarouk amejiuzulu kwa kumuandikia Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson leo Jumapili Julai 21, 2024.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mbarouk amesema amefikia uamuzi huo kufuatia changamoto za kijamii zinazomkabili kwa sasa.
“Ninalazimika kuchukua uamuzi wa kujiuzulu ili nipate nafasi ya kushughulikia changamoto hizo,” amesema Mbarouk katika barua yake ya kujiuzulu Ubunge.
Balozi Mbarouk pia amewahi kuhudumu katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).
Balozi Mbarouk
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇