LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2024

KUWENI MAKINI NA WAUZA MAPORI -RIDHIWANI


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete ameiasa jamii kushiriki katika kufanya uchaguzi wa viongozi wa serikali za Mitaa kwa kuangalia na kuweka mbele uzalendo wao na sio kuchaguana kwa kujuana.

Mhe. Ridhiwani ameyabainisha hayo kwenye Mkutano na Wananchi wa eneo la Mkange Wilayani Chalinze Mkoaji Pwaii ambapo amewasisitiza kushiriki katika hatua zote za uchaguzi kuanzia ngazi ya chini kabisa yakujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura mpaka siku ya kupiga kura katika vituo vutajavyoandaliwa na tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Amesema "hata kama kuna mwanachama wa chama cha Mapinduzi ambaye yeye mwenyewe mnamuona wala hataki mambo hayo ,lakini jamii pale inamtaja vizuri ,mfuateni na mmwambie kama Bwana wewe mwenzetu kila tukikaa Kijiweni tunasema kama kuna mtu mzuri wakutuongoza basi ni Bwana yule pale ambaye ni wewe utatuletea mambo mazuri eneo letu ,basi mfwateni na mwambie ili tukisaidie chama chetu" alisema Mhe.Ridhiwani

"Lakini kutafuta wale marafiki zenu ambao mnauza nao mapori ,kutafuta marafiki zenu mnaofanya nao ubadhilifu wa mali za umma ni kukiingiza chama cha watu kwenye mtihani mkubwa sana", alisema Mhe. Ridhiwani.

Alimaliza kwa kusema kuwa "mimi ninaamini viongozi nyinyi ambao ni wanachama hamtafanya kosa hilo ,tuleteeni watu ambao tukifika hapa watu wanaendelea na shughuli zao tukisubiri siku ya kupiga kura ,tunapiga kura na maisha yanaendelea", alisema Mhe. Ridhiwani.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages