LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 9, 2024

MWENGE WA UHURU WAWASILI IRAMBA DC MWENDA AAHIDI KUULINDA


 Na HEMEDI MUNGA, Iramba 

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleiman Mwenda ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida,  Godwin Gondwe Mkoani hapa.


DC Mwenda ameupokea Mwenge huo wa Uhuru leo katika kijiji cha Maluga wilayani hapa huku akiahidi kuulinda na kuukimbiza kilometa 68.1 ukiwa unawaka, unangaa na kumeremeta kwa muda wote utakaokuwepo Iramba.


Aidha, amedokeza kuwa unatembelea,  kuona, kuweka mawe ya msingi, kupata taarifa mbalimbali ikiwemo kuizindua miradi saba yenye  thamani ya sh bilioni 5.084 ambazo zilitolewa na serikali anayoiongoza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


"Tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, hakika ameitendea haki wilaya yetu kwa sababu katika kila kata kati ya kata 20 za Wilaya hii kuna miradi mikubwa yenye kugharimu fedha nyingi, asante sana Rais wetu," ameshukuru Mwenda.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages