LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 9, 2024

KIONGOZI MKIMBIZA MWENGE WA UHURU KITAIFA AWAPONGEZA WANANCHI IRAMBA


Na HEMEDI MUNGA, Iramba 


WANANCHI wa Wilaya ya  Iramba mkoani Singida ambao wanaongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Suleiman Mwenda wamepongezwa kwa kutafsiri kivitendo falsafa ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhusu viwanda vinavyoongeza thamani na kuzalisha ajira kwa wananchi.


Akizungumza na wananchi wa Kata ya Kyengege wilayani hapa baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda cha Kukamua Mafuta ya Alizeti (Singida Adim Oil Mills) Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava amesema hatua hiyo ni kuyaishi maono ya Rais Dk. Samia nchini.


Amesema Rais Dk. Samia ameendelea kuboresha mazingira ya sekta binafsi, hivyo kuwa rafiki kwa wawekezaji na kufanya biashara.


Ameeleza maelekezo yake ni kuendelea kuona  taasisi zote wezeshi kuhusu  biashara na uwekezaji ziwe rafiki kwa lengo la kuhakikisha zinaendelea kuwavutia wawekezaji na kulinda usalama wa mitaji yao.


"Hakika Rais wetu anafanya hayo kupitia falsafa yake  ya ushirikishaji wa ubia kati ya serikali na sekta binafsi, hivyo nyinyi mmetafsiri maono ya Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan" amesema na kuongeza kuwa:


"Mmeweka mazingira rafiki, hivyo mwenzetu huyu Hamoud Adim ameona  eneo pekee na salama la kuweka mtaji wake ni hapa Iramba."


Hata hiyvo, ameweka wazi  wakulima wa zao la alizeti wamepata uhakika wa mazao wanayo yazalisha kuwa soko la uhakika lipo kwa kuleta katika kiwanda hichi.


Amebainisha kufuatia fursa hiyo, wataweza kulipa kodi ya serikali huku wao wenyewe wakipata kipato kikubwa.


"Mazingira hayo yote, ndio Mheshimiwa Rais Dk. Samia anatamani kuendelea kuyaona ndani ya nchi hii," amesisitiza.


Hata hivyo, amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho Hamoud Adim kwa sababu kiwanda hicho licha ya kutoa huduma kwa wananchi, lakini kimetoa ajira.


Awali akisoma taarifa fupi mbele ya mkimbiza Mwenge huo wa Uhuru Kitaifa, mwakilishi wa mmiliki wa kiwanda hicho, Yasini Mbolole amesema mradi huo umegharimu sh milioni 95.


Mbolole ameongeza kuwa mradi huo unamchango mkubwa wa kuwahudumia wananchi mbalimbali wakiwemo wa kijiji cha Makunda, Kyengege, Mugundu, Kitukutu na Ulemo.


Amefafanua kuwa wananchi wanaweza kuongeza thamani ya mazao kwa wakulima wakubwa na wadogo wadogo huku wakiwa na uhakika wa soko la bidhaa hiyo.


Mbali na hayo, Mbolole amesema mradi huo umechangia kupunguza changamoto ya ukosefu wa  ajira kwa vijana wa maeneo hayo.


Mbio za Mwenge wa Uhuru zimefanikwa 


kutembelea,  kuona, kuweka mawe ya msingi, kupata taarifa mbalimbali ikiwemo kuizindua miradi saba yenye  thamani ya sh bilioni 5.084 ambazo zilitolewa na serikali anayoiongoza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages