LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 17, 2024

MBUNGE LUGANGIRA AMNUSURU MGANE MWENYE WATOTO 6

 

11/7/2024 Mhe Neema Lugangira alipokea wito kutoka kwa Ma Rosemary Stanslaus wa kufika Mtaa wa Nyakanyasi, Kata ya Bakoba, Bukoba Mjini kuangalia namna ya kumsaidia Baba "Makarius Sypirian" Mgane mwenye watoto 6 wadogo. 

Tarehe 13/7/2024 kwa kushirikiana na Dada Rebecca, Afisa Ustawi wa Jamii Kagera wamefika na kwa haraka Mhe Lugangira amefikisha magodoro, vyandarua, blanketi na vyombo ambavyo nilikuwa navyo (shukrani RedCross) na Jumatatu watoto wadogo 2 watapelekwa katika Kituo cha Kulelea Watoto. 

Hakika, Baba huyu anastahili pongezi na msaada, yeye ni mfano wa baba bora; na kupitia picha hizi ambazo baba ameridhia Mhe Neema Lugangira anaomba tumuongezee tabasamu kupitia #NeemaNaMaendeleoFund


Familia ilipokuwa ikilala kabla ya kupatia msaada wa magodoro

Mgane Makarius akiwa na wanawe alioachiwa na mke wake aliyetangulia mbele ya haki.

Lugangira akizungumza jambo na Mgane huyo.
Lugangira akiwanunulia mitumba watoto hao



Watoto wakiwa na furaha baada ya kununuliwa nguo

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages