LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 8, 2024

CHIFU WA WATATURU AMPONGEZA RAIS SAMIA, MIRADI YA NAENDELEO VIJIJINI

NA VICTOR MAKINDA: BUNDA, MARA.


Kiongozi wa Kimila wa kabila la Wataturu  waishio mkoani Mara, Chifu Gituhi,  ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan, kwa kupeleka miradi mingi ya maendeleo vijijini hatua iliyo saidia kupunguza kero  zilizo kuwa zikiwakabili wananchi waishio vijijini.


Gitui ameyasema hayo   Kijijini Sarakwa wilayani  Bunda mkoani mara, wakati alipokuwa akitoa maoni yake  kuhusu uongozi wa Rais Samia kwa muda wa miaka mitatu  tangu alipoingia madarakani.


Amesema  kuwa Rais Samia ameyafanya maisha ya wananchi wa vijijini kuwa bora zaidi kwa kuwa serikali yake imeimarisha huduma za afya, elimu, umeme na maji katika maeneo mengi vijijini. 


Tunamshukuru Mama Samia, ametujengea majosho ya mifugo, mashule na zahanati kila kijiji." Amesema.

Ameongeza kusema kuwa kwa jinsi Rais Samia alivyo imarisha huduma za jamii vijijini ikiwemo miradi ya maendeleo, anamuombea aendelee kutawala mpaka pale ambapo yeye  mwenyewe Rais atakapoona inatosha.

"Mungu akubariki mama, uendelee kuongoza tena na tena mpaka mwenyewe useme basi". Amesema Chifu  Gituhi. 

Akizungumzia kero zilizokuwa zikiwakabili wananchi waishio vijijini husasani jamii za kifugaji amesema kuwa hawakuwa na shule jirani na maeneo yao wala zahanati lakini kwa sasa hudum hizo zinapatikana katika maeneo mengi.  


Msikilize...

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages