Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Nzega Mjini (NZUWASA) mkoani Tabora, imewafikishia huduma ya maji safi na salama wananchi kwa asilimia 99.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa NZUWASA Benadetha Sondo, wakati alipozungumza na CCM Digital mjini Nzega mkoani Tabora.
Sondo alisema kuwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 inaitaka serikali kupitia Wizara ya Maji, kuhakikisha kuwa asilimia 85 ya wananchi waishio vijijini na asilimia 95 ya wananchi waishio mijini wanapata huduma ya maji safi na salama kufikia mwaka 2025 hivyo mamlaka hiyo ilijielekeza kutimiza azma hiyo hatimaye kuvuka lengo.
"Tumevuka lengo, NZUWASA tumefanikiwa kuwafikishia huduma ya maji wakazi wa Nzega mjini kwa asilimia 99". Anasema.
Anaongeza kuwa mwaka wa fedha 2024-25 mamlaka hiyo inatarajia kutoa huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 100 ya wananchi wa Nzega mjini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇