LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 8, 2024

ZIARA YA DK NCHIMBI YAZIDI KUNOGA TANGA

 



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi akizungumza kwenye mkutano wa ndani na Wanachama na Viongozi wa CCM jijini Tanga,  Ijumaa, Juni 7, 2024, ikiwa ni siku ya pili ya hitimisho la ziara yake ya kikazi  ya Mikoa Mitano Mkoa wa  Tanga.


Kabla ya mkutano huo, Balozi Nchimbi alizindua Kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme na kupeleka umeme Vijijini cha Tanga Cable kilichopo mkoani Tanga.


Katika ziara hiyo Katibu  Mkuu wa CCM ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni, Ndugu Issa Usi Haji Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla na Ndugu Rabia Hamid Abdalla, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni, Ndugu Issa Usi Haji Gavu akizungumza kabla ya kumkaribisha Dk. Nchimbi.




 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages