Na HEMEDI MUNGA, Iramba
KATIBU wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Judith laizer ameendelea kutoa elimu inayohusu uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wanawake mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwelewa wa zoezi hilo.
Judith ametoa elimu hiyo, leo wakati akiongea na wanawake wa Kata ya Kyengege wilayani hapa.
Amewaomba kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kwa lengo la kugombea moja ya nafasi zitakazokuwepo kwa sababu kufanya hivyo ni moja kati ya ishara za kuendelea kumuunga mkono Rais wao.
"Niwaombe kila mwanamke kuwa na tabia ya kumuunga mkono mwanamke mwenzake hususan itakapofika muda wa zoezi hilo kwa sababu rafiki wa mwanamke ni mwanamke mwenzake.," amesema.
Aidha, amewataka wanawake hao, kuwachagua viongozi ambao wanakubalika kwa jamii huku akiwaasa kutoogopa kwa sababu kinachohitajika ni moyo tu, nakuendelea kupata uzoefu pole pole sababu hakuna anayezaliwa akiwa ni kiongozi.
Pia, amewaomba kuto wapa nafasi watu ambao wamekua wanajipitisha pitisha katika maeneo mbalimbali ambao hua na tabia ya kuwatumia kwa lengo la kufanikisha mambo yao na baadae wanawaterekeza.
"Niwaombe tushikamane, tuwachague watu wanaokubalika watakao toa ushirikiano wa diwani na mbunge na ifikapo 2025 tumchague Rais Dk. Samia kwa kishindo," amesisitiza.
Amesema wanawake ndio wanaokaa na jamii, hivyo wanao utambuzi mkubwa wa kujua viongozi ambao wanamchango kwa jamiii ikiwemo wananzengo wenzao.
"Ndugu zangu wanawake Rais wetu Dk. Samia anawaamini sana, hivyo mwaka huu na mwakani tuhakikishe tunashinda kwa kishindo,twendeni tukakisaidie Chama cha Mapinduzi kupata viongozi wenye sifa," amesema.
Pia, amewataka wanawake hao, waendelee kumuombea Rais Dk. Samia Suluhu Hassan huku akiwataka kukataa ubaguzi wa ukabila ikiwemo vitendo vyote vitakavyoweza kuleta matabaka.
"Msikubali kuwaunga mkono watu wanaopotosha na kutaka kuharibu amani ya nchii hii," amesisitiza.
Mbali na hayo, amewataka kuunda vikundi vya watu watano watano na kuendelea ambao wanafahamiana wao kwa wao kwa lengo la kwenda kuchukua mikopo itakapotolewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
"Vikundi vyote vitafute miradi na kuvisajili kwa sababu ifikapo mwezi Julai 01, mwaka huu kapu la Mama linafunguka kwa lengo la kuendelea kuwainua wanawake kwa kupata mikopo isiokua na riba," amesisitiza.
Kwa upande wa mmoja wa wanawake hao, Emiliana Kitulo amesema wametoka mbali, hivyo wanashukuru hivi sasa wanayo maendeleo ukilinganisha na siku za nyuma ambapo walitumia mafuta ya myonyo kujipaka mwilini huku wakitumia majani ya mlenda kama sababuni ya kufulia hali ambayo haipo.
Amesema Tanzania ya leo wanashuhudia maendeleo lukuki ikiwemo barabara zenye mataa, huduma za afya maji na umeme hadi katika vitongoji vyao.
Naye Neema John amemuomba Katibu huyo kuwakumbuka wajasiriamali ambao wamekua wakiuza karanga na aadhi ya Mama lishe wapate majiko ya gesi kwa sababu awamu yakwaza hawakubahatika.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Judith laizer akiwataka wanawake kuchangamkia fursa ya mikopo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, baada ya kikao cha ndani kilichofanyika kata ya Kyengege wilayani Iramba mkoani Singida. (Picha na Hemedi Munga)
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Judith laizer akigawa kadi za jumuiya hiyo, baada ya kikao cha ndani kilichofanyika kata ya Kyengege wilayani Iramba mkoani Singida. (Picha na Hemedi Munga)
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Judith laizer akisikiliza baadhi ya hoja za akinamama, baada ya kikao cha ndani kilichofanyika kata ya Kyengege wilayani Iramba mkoani Singida.(Picha na Hemedi Munga)
Baadhi ya wanawake wakifuatilia majibu ya hoja mbalimbali walizoziwasilisha kwa Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Judith laizer, baada ya kikao cha ndani kilichofanyika kata ya Kyengege wilayani Iramba mkoani Singida. (Picha na Hemedi Munga)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇