LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 22, 2024

TIMU YA WAZAWA FC YAICHAPA TOWN STAR


 Na HEMEDI MUNGA, Iramba 


TIMU ya Wazawa FC ya Tarafa ya Kinampanda wilayani Iramba mkoani Singida, imeshinda mabao 3 - 1 dhidi ya Timu ya Town Star ya mjini Kiomboi wilayani hapa.


Pambano hilo, lilikua la ligi ya Pacha Cup 2024 lililofanyika katika uwanja wa Mabatini ikiwa ni mwendelezo wa michezo iliyoanza Juni 16 na kutarajiwa kutamatika mapema mwezi Julai mwaka huu.


Awali kabla ya pambano hilo, Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilayani hapa,  Judith laizer amezipongeza timu hizo kwa kudumisha michezo ambayo sio tu inajenga afya zao lakini ni ajira.


Amesema serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliamua kuwekeza michezo kwa vijana kwa lengo la kuwaepusha na vitendo viovu ikiwemo kuvuta madawa ya kulevya.


"Niwapongeze sana, tunaamini vijana hamtatuangusha," amesema.


Timu ya Town Stara ndio ilikua yakwanza kuandika bao la kuongoza kupitia mchezaji wake Mwalami Sudi kabla ya dakika chache mchezaji wa Wazawa FC, Oza Ndemla kuisawazishia timu yake kupitia mkwaju wa penati.


Aidha, hadi mapumziko timu hizo zilitoka zikiwa suluhu ya bao moja kwa moja.


Kipindi cha pili kimeanza kwa timu zote mbili kupelekeana mashambulizi makali ambayo yalizaa mabao mawili yaliowekwa nyavuni na Ibra Ibrahimu na Denis Jonas wa timu ya Wazawa FC.


Pacha Cup imeandaa zawadi ya mshindi wa kwanza kupata Ng'ombe mbili, mshindi wa pili Ng'ombe mmoja na mshindi wa tatu kupata kitita cha sh 200,000.

Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Judith  laizer akiikagua timu ya Town Star, wakati wa mchezo wa ligi ya Pacha Cup 2024, uliochezwa katika uwanja wa Mabatini mjini Kiomboi. ( Picha na Hemedi Munga)

Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Judith laizer wapili kushoto  akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Yusta Lisu, wakati wa mchezo wa ligi ya Pacha Cup 2024, uliochezwa katika uwanja wa Mabatini mjini Kiomboi. ( Picha na Hemedi Munga)

Timu ya Town Star ya mjini Kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida, ikipeleka mashambulizi dhidi ya Timu ya Wazawa FC ya Misigiri wilayani hapa, wakati wa mchezo wa ligi ya Pacha Cup 2024 uliochezwa katika uwanja wa Mabatini mjini Kiomboi. ( Picha na Hemedi Munga)

Baadhi ya mashabiki wakifurahia bao, wakati wa mchezo wa ligi ya Pacha Cup 2024, uliochezwa katika uwanja wa Mabatini mjini Kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida. ( Picha na Hemedi Munga)




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages