LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 1, 2024

MWANYIKA: SERIKALI IJIKITE KWENYE UJENZI WA MIRADI INAYOCHOCHEA UCHUMI KWA HARAKA


 Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika pamoja na mambo mengine ametilia shaka maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Njombe Mjini- Ludewa ambao anadai unasuasua.


Aidha, ameshauri serikali iangalie jinsi ya kuwasaidia kifedha wakandarasi wazawa ambao kwa hivi sasa baadhi yao wanafilisika na kutotekeleza vizuri miradi.

Pia amesema kuwa serikali ijikite kwenye miradi ya mkakati inayoharakisha uchumi wa nguvu na kwa haraka.

Ametoa mchango wake huo wakati wa mjadala wa makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages